Baadhi ya Viongozi wa Simba wakiteta jambo kwenye Uwanja wa Kaitaba
leo hii jioni, Bila shaka ni swala zima la mtanange wao kesho na Kagera
Sugar huku wakijiuliza maswali kadhaa na kuucheki uwanja wa Kaitaba
jinsi ulivyo katika kipindi hiki. Kocha wa Simba Zdravko Logarusic hakuwepo kabisa kwenye Mazoezi Hapa Kaitaba na inaoneka hakuja na Wachezaji wake. Taarifa zaidi inasemekana atakuja kesho jumamosi siku ya Mtanange. 
Wachezaji wa Simba wakishuka kwenye basi lao kuingia kwenye uwanja wa Kaitaba, Tayari kufanya mazoezi kujiweka fiti na mtanange wa kesho na Wenyeji Kagera Sugar.
Baadhi ya Wachezaji wa Simba wakiingia tayari kwenye nyasi za Kaitaba hapa Bukoba
Tayari kwa mazoezi
Wachezaji wa Simba wakiomba dakika chache kabla ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba jioni
Wachezaji wa Simba wakiteta jambo kabla ya mazoezi, Kipa Ivo Mapunda (katikati) akiwacheki kwa karibu
.
Viongozi wa Simba wakiwacheki vijana wao wakijifua
Kesho tucheka na nyavu tuu
Simba sc wanaingia katika mchezo wa kesho wakiwa hawana cha kupoteza, kwasababu hawahitaji ubingwa wala nafasi ya pili.
Hata hivyo ushindi ni muhimu kwao ili kulinda heshima yao inayozidi kupotea siku za karibuni.
Kagera kwasasa wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 22.

Makipa wote wa Tatu wa Simba wakijifua
Kipa ni Mchezaji muhimu sana kwenye Klabu yoyote ile, na Hapa Ivo Mapunda na mwenzake wanataka ushindi kwani wao ni wazoefu kwenye swala kulinda
No comments: