Taha Basry amefariki dunia Aprili 2, mwaka 2014 katika hospitali ya Cairo alikokuwa amelazwa kwa matibabu akiwa na umri wa miaka 68.
Basry alijiunga na Zamalek mwaka 1965 na alikuwemo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri msimu wa 1977/1978 na Makombe mawili ya Misri mwaka 1975 na 1977.
Alicheza Fainali tatu za kombe la Mataifa ya Afrika katika miaka ya 1970, 1974 na 1976, wakati mwaka 1986 alikuwepo kwenye benchi la Ufundi la Mafarao. Pia aliwahi kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Misri msimu wa 1977/1978. Akiwa kocha, alizifundisha timu za ENPPI, Arab Contractors, Ghazl El-Mahalla na Petrojet.

No comments: