Zile teaser za Weusi zilizokuwa na title ya ‘OTEA’ ambazo wamekuwa wakiziweka kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuanzia wiki iliyopita, tayari imefahamika kuwa ni ujio wa
video ya single yao mpya "Gere".
Nikki
wa Pili wa Weusi amesema kuwa wameshoot video ya ‘Gere’ Nairobi, Kenya
siku chache zilizopita na director Enos Olik aliyefanya video ya Jaguar
‘Kioo’.
Hapo awali ilikuwa inafahamika kuwa kulikuwa na mpango wa video hiyo kufanywa na Nisher, lakini Nikki ameelezea sababu za mabadiliko yaliyojitokeza mpaka kuamua kufanya na Mkenya.
“Bahati
mbaya Nisher alikuwa yuko caught up na mambo mengi na sisi tulikuwa na
haraka so tukashindwa, kwasababu Arusha na Nairobi sio mbali tukavuka tu
boda tu fasta.”
Kama wewe unawafollow Nikki Wa Pili, G-Nako au Joh Makini sina shaka umeshakutana na post kama hii:
"Joh_makini :Otea(gere video) iko tayari kwa yoyote anayetaka xclusive ya siku tano ya video hii..wasiliana na weusi company…." hii ni post ya Joh Makini Instagram.
"Joh_makini :Otea(gere video) iko tayari kwa yoyote anayetaka xclusive ya siku tano ya video hii..wasiliana na weusi company…." hii ni post ya Joh Makini Instagram.

“Hiyo
ni biashara kwa mfano labda kampuni labda Voda au nani tunaweza
tukawapa wakaweka kwenye page yao labda ya Facebook ikawa inapatikana
pale tu”
Nikki ameongeza kuwa video ya ‘Gere’ itatoka wiki ijayo.
Nikki ameongeza kuwa video ya ‘Gere’ itatoka wiki ijayo.
No comments: