Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Wasioona (TLB) Mwalimu Greyson
Mlanga(aliyesimama) akitoa somo juu ya Warsha ya Siku mbili ya Mkatabawa
Umoja wa Mataifa Kwa Watu Wenye Ulemavu Mjini Ifakara hivi karibuni.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Wilaya ya Kilombero Maria Faya na
Kulia ni Mwalimu Janet Kalalu, Mratibu wa Chama Wilaya.
Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Watu wenye Ulemavu nchini Tanzania wametakiwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa muuujibu wa Uwezo wao.
Akizungumza
katika Warsha ya Siku mbili iliyofanyika Mjini Ifakara Wilayani
Kilombero hivi karibuni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona (TLB) Taifa
Mwalimu Greyson Mlanga amesema kuwa ni vyema watu wenye Ulemavu
wakashiriki katika shughuli hizo ili kusaidia Jamiii kuondokana na Dhana
ya kuwa Walemavu ni watu omba omba.
Mwenyekiti
huyo amesema kuwa ushirikiano wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu ndiyo
njia pekee ya kujikwamua katika maisha huku akisisitiza upatikananji wa
Takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu ili ziweze kusaidia maendeleo ya
Watu wenye Ulemavu.
Katika
Mafunzo hayo yaliyoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani,
Watendaji na Wawakilishi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Mwenyekiti
huyo alielezea umuhimu wa kupata Elimu na kujua Haki za Watu wenye
Ulemavu.
Mafunzo
hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wasioona (TLB) Wilaya ya Kilombero
yameshirikisha Wadau kutoka Kata za Ifakara, Kibaoni, Kiberege na
Kisawasawa yalifadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society.
Viongozi
wa TLB Taifa Wakiungana na Viongozi wa TLB Wilaya ya Kilombero katika
kuimba Wimbo wa Haki za Binadamu katika Mafunzo ya Siku Mbili
yaliyowakutanisha Wadau mbalimbali, Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Wilaya
ya Kilombero, uliofanyika hivi karibuni Mjini Ifakara. Kutoka Kushoto ni
Maria Faya, Mwenyekiti wa TLB Wilaya ya Kilombero Maria Faya, Mwalimu
Robert Bundala,Makamu Mwenyekiti Wasioona Taifa, Mwenyekiti wasiona
Taifa Mwalimu Greyson Mlanga na Mratibu wa Wasioona Wilaya ya Kilombero
Mwalimu Janet Kalalu.
Washiriki wa Mafunzo ya Siku Mbili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa Juu ya Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Viongozi wa Taifa wa Chama cha Wasiona (TLB) Mjini Ifakara Hivi karibuni.
PICHA NA HENRY BERNARD MWAKIFUNA
No comments: