Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akieleza kwa waandishi wa Habari
(hawapo pichani) kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato unatumiwa na manispaa hiyo,wakati wa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara
ya Habari(MAELEZO) Fatma Salum.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa Bw.
Jackson Kiema akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) mashine ya
kielektroniki inayotumika katika ukusanyaji wa mapato na kuhifadhi taarifa za
mapato, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera. PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
====== ====== =====
MFUMO
MPYA WA UKUSANYAJI WA MAPATO
Kutokana na
kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini, Manispaa ya Kinondoni imeanzisha
utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na
Max-malipo.
Huduma hiyo
mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,humwezesha
mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.
Huduma hii
inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama
“Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34
imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.
Mfumo huu wa
ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia
maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa
huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.
Kimsingi
hatua hii inahamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika utoaji wa maamuzi
yanayohusu mambo yao na kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi, inayowajibika
na makini katika kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
Hivyo basi
kutokana na malengo na umuhimu wa kuwarahisishia wananchi, Manispaa iliona ni vema
ikaingia haraka ndani ya utaratibu huu ili Mwananchi aweze kulipia kodi popote
kwa kutumia Max-malipo au wakala wa
simu za mkononi yaani Tigo pesa Na. 212888 na M-Pesa Na. 212888.
MAFANIKIO
YALIYOPATIKANA.
Katika
kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa
na mafanikio makubwa kama ifuatavyo:-
·
Mapato yameongezeka kwa kiwango
kikubwa mfano; ada ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka
kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa
na ongezeko LA 69%
·
Chanzo cha kodi ya majengo hadi
mwishoni mwa Machi tulikusanya Tshs.
339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013
tulikusanya sawa na ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=
·
Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi
bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za
jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18%
·
Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa
wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.
·
Lesseni za biashara hadi Machi
tumekusanya Tshs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki
ya Tshs. 2.6 Bilioni kwa mwaka.
Napenda
kuwahakikishia wananchi wa Kinondoni kuwa Manispaa ya Kinondoni itazidi
kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwawezesha
kuwa na maisha bora kutokana na mafanikio haya, lipa.
Lipa kodi
kwa maendeleo ya Manispaa yako.
IMETOLEWA NA
SEBASTIAN
MODESTUS MHOWERA
AFISA
UHUSIANO WA MANISPAA
HALMASHAURI
YA MANISPAA YA KINONDONI
SIMU
NA:
0754-227024
No comments: