Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kati) akiendesha duwa rasmi ya
kuwaombea viongozi waasisi wa Muungano ambao wametangulia mbele za haki
kama wanavyonekana kwenye picha Hayati Mwalim Julius K. Nyerere na
Hayati Abeid Amani Karume muda mfupi baada ya kupokea msafara wa mbio
hizi ofisini kwake jana tarehe 07-04-2014.
Msafara
wa Mbio za Uzalendo Tanzania ukiondoka katika Ofisi ya Mkuu ya Mkoa wa
Rukwa mara baada ya kupata baraka za kiongozi huyo na kusaini kitabu
tayari kwa zoezi la mbio hizo katika Manispaa ya Sumbawanga na baadae
kuelekea katika Mji Mdogo wa Laela.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiondoka na pikipiki iliyokuwa
ikiendeshwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Philipo Elieza
ambapo alishiriki mbio hizo hadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
nje ya uwanja wa Nelson Mandela katikati ya Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongoza mbio hizo na vijana wa UVCCM kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Mb) akizungumza katika
Mkutano wa hadhara ambapo alisema tunu ya muungano ni lazma ilindwe na
kila moja wetu na kuwa sio jambo la hiari. Aliongeza kuwa madai ya uwepo
wa Serikali tatu ni hatua za kuhatarisha Muungano uliopo wa Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar hivyo hakuna budi kuimarisha Muungano wa
Serikali mbili kwa maslahi watanzania wote. Aliuotelea mfano muungano wa
Serikali tatu kuwa hauna tofauti na kuchukua kisu na kugawana mtoto
ambapo kila mzazi atachukua kipande ambacho sio mtoto kamili.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Katibu wa UVCCM
Mkoa wa Rukwa Ndugu Philipo Elieza cheti cha pongezi kwa ushiriki wa
Mbio za Uzalendo Tanzania na kingine kwa UVCCM Mkoa na Taifa kwa kuandaa
na kufanikisha mbio hizo. Mkuu huyo wa Mkoa aliandaa vyeti vya pongezi
kwa washiriki wote wa mbio hizo.
Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Agustino Mzurikwao akitoa salam za vijana
wa CCM katika mkutano huo wa hadhara ambapo alisisitiza juu ya vijana
kutumia fursa zilizopo katika kujiendeleza kiuchumi na kudumisha
Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Kulia ni Katibu Muenezi
wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RukwaMkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea msafara wa pikipiki wa vijana wa CCM (UVCCM) ambao wanaendesha mbio za Uzalendo Tanzania zikiwa na lengo la kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar jana tarehe 07-04-2014. Mbio hizo za kitaifa zinahusisha msafara wa pikipiki tano zinazoongozwa na viongozi watatu wa UVCCM ambao wanakuwa kwenye gari, aidha zinashirikisha wadau mbalimbali wa UVCCM katika kuzifanikisha. Mbio hizo zinahimiza vijana kudumisha muungano, kuweka utaifa mbele na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao. Mbio hizo zitakuwa Mkoani Rukwa tarehe 07 na 08 April 2014 na kuelekea Mkoani Mbeya.
No comments: