Mfanyakazi
wa kampuni ya Fusun Investment Co. United akifanyakazi katika moja ya
mashine zinazotumika katika usagaji wa chupa chakavu za plastiki kabla
ya kusafirishwa nchi za nje. Kampuni hiyo imetoa ajira zaidi ya 300
tangu ilipoanzishwa mwaka 2010, na inampango wa kujitanua katika mikoa
mingine Tanzania.
Mfanyakazi
wa kampuni ya Fusun Investment Co. United Limited akikusanya chupa
chakavu za plastiki kwa ajili ya kuzisaga. Zaidi ya watanzania 300
wanafanyakazi katika kampuni hiyo ya kichina ambayo ukusanya chupa
chakavu zaidi ya tani 700 kwa mwezi. Kampuni hiyo imesema inampango wa
kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.
Lundo
la chupa chakavu za plastiki zikisubiria kusagwasagwa na kiwanda cha
Fusun Investment Co. United Limited kilichopo Kurasini jijini Dar es
Salaam. Kampuni hiyo ya kichina ukusanya chupa chakavu zaidi ya tani 700
kwa mwezi, na kwa sasa inampango wa kujitanua katika mikoa mingine
Tanzania.
Lori
lililobeba chupa chakavu za plastiki likiwa tayari kushusha chupa hizo
kwa ajili ya kusagwa katika kiwanda cha Fusun Investment Co. United
Limited kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ya kichina
ukusanya chupa chakavu zaidi ya tani 700 kwa mwezi, na kwa sasa
inampango wa kujitanua katika mikoa mingine Tanzania.
KAMPUNI
ya kuhuisha (recycling) plastiki ya kichina inayofanya shughuli zake
jijini Dar es Salaam ina mpango wa kutanua shughuli zake kwa kuwekeza
zaidi nchini na kuongeza ajira zaidi kwa watanzania.
Kampuni
hiyo, Fusun Investment Co. United Limited imesema jijini Dar es Salaam
jana wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda cha kampuni
hiyo kilichopo Kurasini, kuwa ajira zaidi ya 300 zimeshatolewa mpaka
sasa.
“Wakati
biashara yetu ikiendelea kutanuka, kuna uwezekano mkubwa wa sisi kuweza
kuajiri watu wengi zaidi,” alisema Bw. Jiang Jiaxing, Mkurugenzi wa
kampuni hiyo.
Alisema
kuwa kampuni hiyo iliyoanzishwa tangu Desemba mwaka 2010 inakusanya
tani 700 ya chupa za plastiki toka mtaani kwa wananchi kila mwezi na
kuzisaga kuwa chakavu na kuzisafirisha nchini China kwa ajili ya
kutengeneza vifaa vya plastiki vipya.
Pia,
alisema kuwa kampuni yake imefungua viwanda viwili vilivyopo katika
maeneo ya Mabibo na Mikocheni jijini Dar es Salaam na mipango zaidi
inafanyika ya kujitanua shughuli zake zaidi katika mikoa mingine
vijijini.
“Tumechangia
katika uchumi wa Tanzania kwa njia nyingi kama vile kuingizia nchini
fedha za kigeni, mapato kwa njia ya malipo ya kodi na ushuru pamoja na
kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira kwa kukusanya
plastiki zinazo zagaa ovyo kisha kuhuisha,” alisema na kuongeza:
“Hebu
tafakari, nini kingeweza kutokea endapo tani 700 za chupa chakavu za
plastiki zingeachwa zikizagaa mitaani?. Ingelikuwa ni tatizo kubwa”.
Ripoti
za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Dar es Salaam inakumbwa na tatizo
kubwa la utunzaji wa takataka ngumu. Ikiwa ni jiji la tatu linalokua kwa
kasi katika nchi za Jangwa la Sahara na la tisa duniani, linakumbana na
changamoto kubwa ya jinsi gani ya kutunza taka zinazozalishwa.
Tafiti
zilizofanyika katika miaka ya 1980 zilionyesha kuwa jiji la Dar es
Salaam linazalisha zaidi ya tani 1,200 ya taka ngumu kila siku, lakini
tafiti za hivi karibuni zinaonyesha taka zizalishwazo jijini kwa sasa
zimeongeza kwa zaidi ya tani 2,500 kwa siku. Jiji halina miundombinu ya kutosha inayohitajika katika kushughulikia ongezeko la taka ngumu na wingi wa taka maji zilizopo.
Tatizo
la utunzaji taka la jijini Dar es Salaam linalenga zaidi utupaji wa
taka na usafi wa mazingira, takataka zisizokusanywa zikiachwa zimezagaa
mitaani,au kuchomwa moto kiholela katika kona mbali mbali za mitaa.
Changamoto hasa ni katika maeneo ya mijini ambayo yamekuwa yakiongezeka zaidi katika miaka michache iliyopita. Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1965, miaka michache baada ya uhuru na
leo idadi ya wakazi wa mijini nchini Tanzania imeongezeka kutoka
asilimia 5.0 mpaka zaidi ya asilimia 36 kwa sasa. Mlipuko huu wa ukuaji
wa miji hauendani na uwezo wa kuzikabili taka zinazozalishwa.
No comments: