Malori
na Mabasi yakiwa kwenye msongamano baada ya kushindwa kuendelea na
safari kwa takribani masaa zaidi ya nane katika eneo la Manzese lililopo
Kilwa barabara ya Dar Es salaam kuelekea Mtwara, jana kutokana na eneo
hilo kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea
magari zaidi ya mia kukwama katika eneo hilo.
Baadhi
ya wasafiri kwenye mabasi yaendayo Dar Es Salaam kutoka Mtwara, Lindi
na Kilwa na yale yatokayo Jijini Dar Es Salaam kuekelea mikoa ya Kusini
wakiwa wamesimama kushuhudia juhudi zinazofanya na vijana wa eneo la
Manzese na baadhi ya madereva wa malori na mabasi pamoja na abiria
kuhakikisha wanasaidia magari kuvuka ili kuweza kuendelea na safari zao.
Wasafiri
na wakazi wa Eneo la Manzese wakishuhudia greda lililofika kwaajili ya
kusaidia kusawazisha eneo hilo na kutoa magari yaliyonasa kutokana na
eneo hilo kujaa maji na tope zito yaliyosababisha magari kukwama kwa
takribani masaa zaidi ya nane hapo jana.
Mabasi
yatokeayo Mikoa ya Kusini kuelekea Bara yakiwa yamekwama katika eneo la
Manzese - Kilwa kutokana na barabara kuwa mbovu katika eneo hilo
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kusababisha magari
zaidi ya mia kunasa na kutoendelea na safari zao kwa zaidi ya masaa
nane.
Greda
likiondoa tope na kusawazisha eneo hilo ambalo lilileta usumbufu mkubwa
sana kwa watumiaji wa barabara ya Dar Mtwara na kupelekea magari zaidi
ya mia kukwama katika eneo hilo lililoaharibiwa na mvua zinazoendelea
kunyesha. Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Malori yakiwa kwenye msururu.
No comments: