Beki
na nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic ameagwa rasmi leo Old
Trafford baada ya kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa
nyumbani msimu huu na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Hull City.
Vidic amepewa zawadi ya shukurani kwa utumishi wake wa miaka nane katika klabu hiyo, huku akiwa tayari alishaaga.
Beki huyo alipewa zawadi hiyo na Sir Bobby Charlton kabla ya vijana wa Ryan Giggs hawajaanza mechi.
Hata
kama beki huyo mwenye miaka 32 alianzia benchi katika mechi ya leo,
lakini alipata nafasi ya kucheza kwa mara ya mwisho Old Trafford.
Tabasamu: Nemanja Vidic alipewa zawadi na Sir Bobby Charlton usiku huu Old Trafford
Kwaheri: Beki huyu wa kati anaondoka mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na klabu ya Inter Milan
Mshangao: Vidic alianzia benchi dhidi ya Hull City, lakini aliingia baada ya Phil Jones kuumia.
Jones aliumia dakika za mwanzo na kumpatia Mserbia huyo nafasi ya kucheza mechi yake ya mwisho Old Trafford.
Giggs
aliweka mipango ya kumchezesha Vidic ili kuwaaga mashabiki wa Man
United baada ya utumishi wake uliotukuka wa miaka 8 akitokea klabu ya
Spartak Moscow mwaka 2006.
Beki
huyo akiwa na Man United ameshinda mataji matano ya ligi kuu, kombe la
UEFA na makombe matatu ya ligi chini ya kocha aliyestaafu Sir Alex
Ferguson.
Kwa mara ya mwisho, Vidic alianzia benchi Old Trafford
No comments: