KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetoa
msaada kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela kufuatia mafuriko yaliyoikumba Wilaya
hiyo hivi karibuni na kutoa athari kubwa kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada
huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Ester Malenga, Mkuu wa Kitengo cha
Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya
kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna
ya kutoa msaada kwa waathirika hao.
Alisema baada ya kuchangishana na kupata
shilingi Milioni 10, walikubaliana na kitengo cha Msalaba Mwekundu juu ya vitu
vinavyohitajika kwa haraka kwa ajili ya kuwapa msaada waathirika na ndipo
walipowakabidhi fedha hizo.
Alisema Msalaba mwekundu walinunua
Magodoro 500, Vyandarua 500 na mablanketi 500 vyote vyente thamani ya shilingi
Milioni 10 ambavyo viliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela juzi.
Aidha Mwakifulefule alitoa wito kwa
mashirika mengine kujitolea kwa hali na mali misaada mbali mbali kwa wakazi wa
Wilaya ya Kyela kutokana na kuwa bado na mahitaji muhimu.
Alisema hali badi ni tete na maeneo
mengi yaliyoathirika bado hayajafikiwa hivyo ni vema taasisi zingine
zikajitokeza kusaidia wananchi walioathirika na mafurika hayo.
Kwa upande waku Mkuu wa Wilaya ya Kyela,
Margareth Esther Malenga, akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi alitoa
shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada
walioutoa wananchi wake.
Alisema Kampuni ya Vodacom inaubia na
Serikali lakini ndani yake imekuwa ikiitumikia jamii na wananchi ambao ndiyo
wateja wao na watumiaji wa bidhaa zao lakini wanaguswa na kutoa misaada mbali
mbali kwa jamii inapokuwa inahitajika.
|
No comments: